Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuutaarifu umma
kuwa imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma
stashahada (Diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 kama
ilivyotangaza awali.
Itakumbukwa
kuwa tarehe 10 Mei mwaka huu, HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji
mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Mwongozo huo, pamoja na mambo
mengine, unaeleza kuwa HESLB itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa
stashahada na kuwa mwongozo kuhusu utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ya
wanafunzi wa stashahada ungetolewa baadae.
Hatua
hii imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa kiasi chote cha TZS 427.5 bilioni
zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2018/2019
zinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya
wahitaji ambao wana sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndiyo
walengwa wakuu.
Hivyo
basi, tunatoa wito kwa wanafuzi wote wenye sifa za kujiunga na masomo
ya shahada katika taasisi za elimu ya juu na ambao ni wahitaji wa mikopo
kuhakikisha wanasoma kwa makini mwongozo wa utoaji mikopo na
kuuzingatia.
Kwa
takwimu za mwaka 2017/2018, takribani maombi 10,027 ya mikopo
yaliyowasilishwa Bodi ya Mikopo yalikuwa na upungufu kama vile
kutosainiwa, kutokuwa na viambatanisho sahihi n.k.
HESLB
ilianzishwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi
Julai, 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na pia kukusanya
mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
0 comments:
Chapisha Maoni