Kamati
ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, imeishauri serikali kurudisha
jukumu la ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa serikali za mitaa.
Makamu
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni amesema wanatoa ushauri huo kwa
sababu bado Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) haijawa na uwezo wa kutosha
kukusanya chanzo hicho.
Makamu Mwenyekiti huyo amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango.
“Kamati
inaishauri serikali kurudisha chanzo hiki katika mamlaka ya serikali za
mitaa kwa sababu bado mamlaka ya mapato haijawa na uwezo wa kutosha
kukusanya chanzo hiki.
“Pili
ni utaratibu wa kutumia dhamana ya serikali za mitaa katika kupata
fedha za maendeleo kwa serikali za mitaa utashindikana kwa sababu
halmashauri hazitakuwa na uwezo wa kulipa riba pindi amana hizo
zinapoiva.
“Tatu
kamati inaishauri serikali kutumia wanafunzi wa Chuo cha Ardhi kufanya
shughuli ya kufanya tathimini ya majengo wakati wa mafunzi ya vitendo
ili kuongeza tija ya ukusanyaji wa mapato husika,” amesema.
Aidha
amesema tathimini ya ujumla ya mwenendo wa utaoaji wa fedha za
utekelezaji bajeti ya mwaka 2017/18 si wa kuridhisha kwa baadhi ya
mafungu.
“Hadi
kufikia Machi mwaka huu kati ya mafungu nane yaliyo chini ya Wizara ya
Fedha, ni mafungu mawili tu yalikuwa yamepokea fedha zaidi ya asilimia
60 ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni