WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inasimamia kwa karibu miundombinu
ya elimu nchini, malezi na nidhamu ili kuhakikisha kunakuwa na usawa
katika ngazi zote.
Ametoa
kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma
katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati
akijibu swali la Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajab aliyetaka kujua
Serikali imechukua hatua gani kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa
kwenye shule binafsi ikiwemo nidhamu na malezi.
Waziri
Mkuu amesema licha ya kuwa Serikali imetoa fursa ya uwekezaji kwenye
sekta ya elimu na kuruhusu watu binafsi waweze kuendesha shule au vyuo,
haina maana kuwa kila mtu ana uwezo wa kuendesha shule kadri apendavyo.
Amesema
Serikali inasimamia kwa karibu miundombinu ili kuona kama inakidhi
mahitaji ya taasisi iliyokusudiwa; inachunguza kama imesajiliwa;
inafanya ukaguzi wa mazingira ya mahali taasisi ilipo, iloi kubaini kama
ina eneo la kutosha na mazingira hayo yanaruhusu kutolea taaluma.
“Jambo
jingine ambalo tunasisitiza ni kwamba; kama mwekezaji huyo amekubali
kuwekeza kwenye elimu ya msingi, sekondari au chuo, atalazimika kufuata
mitaala ya kiserikali; ili afundishe mtaala ambao pia unafundishwa
kwenye shule za Serikali na watoto wote wapate elimu inayofanana,”
amesema Waziri Mkuu.
Amesema
Serikali inafanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini kama elimu
inayotolewa na taasisi husika ina kiwango sawa na taasisi nyingine kwa
sababu mwishoni kuna mitihani inayotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa
ili kupima kama elimu waliyoipata inafuata mtaala mmoja na kama ina
viwango vinavyotakiwa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu suala la malezi na nidhamu, Waziri Mkuu amesema suala
hilo linawekewa msisitizo kwa sababu ndilo linajenga vijana ambao
watakuwa viongozi wa baadaye. “Lengo letu ni kuona elimu inaboreshwa,
inawiana kote nchini na wawekezaji wanakaguliwa ili kutotofautisha
viwango na ubora wa elimu inayotolewa nchini,” amesema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Chapisha Maoni