Australia
nayo imewafukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana
na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei
Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.
Waziri
mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari
la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara
mwisho vita vya pili vya dunia.
Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia.
Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.
Donald Trump amesema Urusi inapaswa kuachana na tabia zake hatarishi kwa mataifa mengine
Waziri
wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema hatua hiyo ya nchi
nyingine kuungana na Uingereza ni matokeo ya tabia ya Urusi kuingilia
nchi za watu.
''Ambacho
kimesababisha nchi zote hizi kuungana na sisi, ni kutokana na vitu
ambayo urusi imefanya, nchi nyingi ndani ya miaka kumi wameshuhudia kama
sio jaribio la mauaji kufanyika nchini mwao basi wameingiliwa katika
uchaguzi wao na mitandao yao, aina zote za tabia zisizo kubalika za
Urusi,'' alisema Johnson.
Seneta wa Urusi Andrey Klimov anasema kuwa hakuna ukweli wowote wa shutuma dhidi ya Urusi bali ni propaganda dhidi yao.
Iceland
imetangaza pia itasimamisha mazungumzo na mamlaka za Urusi na viongozi
wake hawatahudhuria michuano ya kombe la dunia mwezi wa sita.
Mapema Uingereza ilisema kuwa hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la dunia.
Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.
Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.
0 comments:
Chapisha Maoni