WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekemea uharibifu wa makusudi wa miundombinu ya
barabara na majengo unaofanywa na baadhi ya wananchi na kuwataka waache
tabia hiyo mara moja.
Ametoa
kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma
katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati
akijibu swali la Mbunge wa Magu, Bw. Kiswaga Destery aliyetaka kujua
Serikali inachukua hatua gani dhidi ya wananchi wanaoharibu miundombinu
ili wakauze kama vyuma chakavu kwa vile Serikali inatumia fedha nyingi
kujenga miundombinu hiyo.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inatumia fedha nyingi sana kuboresha miundombinu
mbalimbali nchini na kwamba kila Mtanzania anao wajibu wa kulinda
miundombinu hiyo.
“Serikali
inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya barabara na majengo ili
kutolea huduma, Watanzania wote tunao wajibu wa kuilinda na endapo
itatokea mtu anaihujumu miundombinu hii, Serikali hatuwezi kukaa kimya,
lazima tutachukua hatua,” ameonya.
Amesema
jukumu la ulinzi ni la Watanzania wote, na kila Mtanzania anayo dhamana
ya ulinzi na usalama wa ndani ya nchi ikiwemo kuilinda miundombinu.
“Juzi niliona kwenye televisheni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
TAMISEMI, Mheshimiwa Jaffo akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama
mkoani Shinyanga, wamekamata Fuso lililojazwa vyuma vilivyong’olewa
kwenye barabara, ni vile ambavyo vinawekwa kwenye daraja na kingo za
barabara,” amesema.
“Huu
ni uharibifu ambao hatuwezi kuvumilia, na katika hili Watanzania lazima
tuungane pamoja tukemee tabia hii. Tunatumia fedha nyingi kujenga kingo
za barabara, kuashiria maeneo yenye hatari lakini Watanzania wengine
wanakuja kung’oa kwa matumizi yao. Mimi naamini Mkoa wa Shinyanga
utakuwa umechukua hatua kali dhidi yao,” amesema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Chapisha Maoni