Mahakama
ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya
Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga
kuugua ghafla.
Kabla
ya kuhairishwa kwa kesi hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa
mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Sunday Hyera ulionekana
kutokubaliana na taarifa hizo za ugonjwa.
Hali
hiyo ilimfanya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka
mdhamini pamoja na wakili wa upande wa utetezi, Barthelomew Tarimo
kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha taarifa hizo za
ugonjwa.
Wakili
Tarimo na mdhamini wa Kiwanga walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo
ya daktari wa kituo cha afya cha Aga khan iliyoeleza kuwa Kiwanga
anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na kuiwasilisha mahakamani.
Katika
taarifa hiyo ya daktari ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita
na hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu.
0 comments:
Chapisha Maoni