Wanachama
wa Vyama vya Ushirika nchini wametakiwa kuacha kuchanganya mambo ya
siasa na ushirika ili kuondoa migogoro na migongano inayotokea mara kwa
mara katika vyama vyao.
Kaimu
Mrajisi ushirika huo nchini, Tito Haule ametoa rai hiyo leo wakati
akizungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika (RUNALI)
kinachokutanisha wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale mkoani Lindi.
Haule
amesema kuna tabia ya baadhi ya wanachama wa vyama vya ushirika
kuchanganya mambo ya kisiasa na ushirika jambo lilonasababisha migogoro
ndani ya vyama vyao na kubadilisha dhana na malengo ya ushirika ya
kuwaunganisha wakulima pamoja.
“Lengo
la kuanzisha ushirika ni kuwaunganisha wakulima kuwa na sauti moja ili
kuweza kupanga bei ya mazao na kuzuia mianya ya walanguzi, shida kubwa
wana ushirika hasa kusini ni kuchanaganya masuala ya uchumi na maslahi
kisha wanachagua viongozi kwa ushabiki,” amesema Haule.
Kwa
upande wake Salima Chilima kutoka Chama cha Msingi cha Muungano
(AMCOS), alisema suala hilo la kuchanganya siasa na shughuli za ushirika
linawafanya wanaushirika kugwanyika kutokana na itikadi za vyama vyao.
0 comments:
Chapisha Maoni