Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema hali
ya usalama ya Jiji hilo ni shwari huku akielezea matukio kadhaa ambayo
yametokea katika kukabiliana na matukio ya uhalifu.
Mambosasa
amezungumza jana jijini Dar es Salaam ambapo ameelezea pia kukamatwa
kwa watu 10 wanaotuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.
Amewataja
watuhumiwa hao ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Ismaili
(18) mkazi wa Tandika, Issa Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18)
mkazi wa Tandika, Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika, na watano
wengine ambao majina yao wameyahifadhi kwa sababu za kiupelelezi.
Mambosasa
amesema Aprili 29 mwaka huu, saa sita usiku katika maeneo ya Tandika
Foma askari wakiwa doria waliitilia shaka gari namba T 401 CLF aina ya
Toyota Alteza rangi ya fedha na kuanza kulifuatilia kisha kulikamata na
kukuta watu watano wakiwa ndani ya gari hilo.
Amefafanua
askari waliwaweka chini ya ulinzi watu hao na kufanya upekuzi ndani ya
gari hilo na kufanikiwa kukamata Bastola aina ya Browning yenye namba
N635BRE ikiwa na risasi mbili ndani ya Magazine ikiwa na Watuhumiwa
waliokamatwa kwenye gari hiyo ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika,
Mohamed Isimaili (18) mkazi wa Tandika, Issa Saidi (19) mkazi wa Yombo,
Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika na Shabani Nassoro (17) mkazi wa
Tandika.
"Watuhumiwa
hao walihojiwa na mtumiwa mmoja Bushiri Ally alikiri bastola hiyo ni ya
kwake na aliiokota Tandika mtaa wa Mteja mwaka 2014 na huwa anaitumia
kufanyia vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji,"amesema.
Katika
tukio lingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kukutwa na Bastola 2 na
risasi 16, nyundo moja na bisisi tatu ambavyo walikuwa wakivitumia
katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa wizi wa magari hapa Jijini.
Amesema
watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea
kufanyika dhidi ya wezi wa magari na wahalifu wanaotumia silaha.
Aidha
ameeleza Mei 5 mwaka huu, saa tano usiku maeneo ya Mbezi Makondeko
Remmy Wilbard (41) mkazi wa maeneo hayo akiwa anatoka kwenye biashara
zake na gari Toyota Noah namba T681 DJM rangi ya fedha.
Amesema
na alipofika nyumbani kwake alishuka kwenye gari lake kwaajili ya
kwenda kufungua geti, ghafla alivamiwa na watu watatu wakiwa na bastola
moja na silaha za jadi na kumpora gari hilo.
"Mlalamikaji
alifungua kesi katika kituo cha Polisi Kimara na upelelezi ulianza mara
moja ambapo Mei 7 mwaka 2018, saa 12 jioni Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es salaam lilipata taarifa kutoka msiri wake kuwa huko Sinza
Kumekucha kuna watu wanataka kuuza gari la wizi.
Amesema
ulifanyika ufuatiliaji na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili, na
baada ya kufanya mahojiano ya kina na watuhumiwa hao yalipelekea
kuwakamata watuhumiwa wengine watatu.
Baada
ya kukamilisha mahojiano na watuhumiwa hao watano Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es salaam liliongozana na watuhumiwa hao hadi kwenye makazi
yao na kufanya upekuzi.
Hivyo
Mei 8 mwaka huu maeneo ya Kimara King’ong’o Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam lilienda mpaka kwenye nyumba ya mtuhumiwa wa
kwanza na kufanya upekuzi na kufanikiwa kupata silaha bastola ambayo
haijatambulika aina yake yenye namba AK-0383 TZCAR 71414 iliyokuwa
imefichwa ndani ya kabati la nguo ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.
Ameongeza
kuwa Mei 10 mwaka huu , saa tano usiku maeneo ya Mbagala rangi tatu
alikamatwa mtuhumiwa mwingine baada ya kufanyiwa Upekuzi katika nyumba
anayoishi alikutwa na silaha bastola aina ya Beretta U.S.A CORP.
ACOOKEEK.MD ikiwa imefutwa namba na risasi sita ndani ya magazine.
"Watuhumiwa
hao walikiri kujihusisha na wizi wa magari na uhalifu wa kutumia silaha
katika maeneo ya Jiji.Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zao hivi,"amesema.
Kuhusu
hali ya usalama barabarani Mambosasa amesema kuanzia Aprili 14 mwaka
hadi Mei 10 mwaka huu kikosi cha usalama barabarani kinaendelea na
juhudi za kupunguza ajali za barabarani kwa kufanya ukaguzi na ukamataji
magari na pikipiki mbovu.
Amesema
katika kipindi hicho jumla ya magari yaliyokamatwa ni 44,879 idadi ya
pikipiki zilizokamatwa 1,466, idadi ya daladala zilizokamatwa ni 17,199,
idadi ya magari mengine (binafsi na malori) ni 27,680 na bodaboda
waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia
mshikaki ni 103,hivyo jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 125,456. Fedha
zilizopatikana kutokana na makosa ya usalama barabarani ni jumla ya
Sh.1, 563,082,500.
0 comments:
Chapisha Maoni