Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuadimika
kwa bidhaa muhimu ya sukari ilikuwa ni propaganda kwa sababu ipo ya
kutosha.
Pia
amesema masuala ya propaganda anayafahamu vya kutosha kwa sababu
amesomea kutoka China na kufunzwa na mwanasiasa mkongwe marehemu
Kingunge Ngombale Mwiru.
Mwijage
ametoa kauli hiyo jana Mei 11 wakati akijibu hoja za wabunge
waliochangia mjadala kuhusu bajeti yake kwa mwaka 2018/19 na kuongeza
kuwa suala la uhaba wa sukari, yeye ni mcha Mungu pia aliyekuwa mama
yake na bibi walikuwa waislamu hivyo hawezi kuwahujumu Waislamu katika
kipindi hiki cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Watanzania
niwaambie tunayo sukari ya kutosha, kuna tani 45,000 kwenye stoo,
Tanzania tunatumia 40,000 kwa mwezi, lakini bandarini nimemwagiza TBS
(Shirika la Viwango) na TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa) sukari
iliyopo bandarini itoke. Mbunge wa kwanza ameniambia nimpe tani 1,000.
Wabunge njooni mchukue sukari tunayo ya kutosha bandarini tani 22,000
zipo tayari.
“Mbali
na sukari hiyo, viwanda vyote vya sukari vimebakisha wiki tatu hadi
hadi vianze kuzalisha kwa hiyo suala la uadimikaji wa sukari lilikuwa
propaganda na katika propaganda mimi nimesomea mpaka China. Ilikuwa
propaganda, sukari ipo, kama ni propaganda, propagandist mwenyewe ni
mimi. Kama Mzee Kingunge Ngombale Mwiru mngemuuliza kwa sababu
alinifundisha yeye.
“Kwa
hiyo hakuna tatizo la sukari, niko hapa na tunafunga kwenye mwezi
Mtukufu wa Ramadhani atakayekuwa na tatizo aje aniulize. Tunasambaza
sukari kwenda mikoani,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni