Jeshi la Polisi nchini limewaaga makamishna wa Polisi wawili ambao wamefikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Makamishna hao ni aliyekuwa Kamishna wa Polisi wa Fedha na Lojistiki, Clodwin Mtweve ambaye baadaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza nafasi ambayo ameitumikia hadi kustaafu kwake.
Mwingine
ni aliyekuwa Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi wa Makosa
ya Jinai, Alice Mapunda ambaye ndiye polisi wa kike wa kwanza
kupandishwa cheo hadi kufikia cheo cha Kamishna kwa Jeshi la Polisi
tangu uhuru.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema
kuwa katika utumishi wao ndani na nje ya Jeshi la Polisi Makamishna hao
walishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kushiriki kikamilifu katika
operesheni mbalimbali za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa na kuliletea sifa
Jeshi la Polisi Tanzania ndani na nje ya nchi.
Kutokana
na mchango wao kwa taifa, makamishna hao wametakiwa kuendelea kuwa
msaada kwa Jeshi la Polisi wakati wowote watakapohitajika kwa kutoa
ushirikiano na ushauri wa kitaalam utakaosaidia kupunguza uhalifu hapa
nchini.
Hafla
ya kuwaaga makamishna hao imefanyika jana katika Chuo cha Taaluma ya
Polisi Dar es Salaam (DPA) kilichopo Kurasini kuanzia saa moja na nusu
na palipambwa na gwaride na mayonesho mbalimbali ya kazi za Polisi.
Wastaafu hao Clodwin Mtweve na Alice Mapunda.
0 comments:
Chapisha Maoni