Ofisa
Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clifford, Razack Hamad (26) amefikishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kuchapisha
taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram.
Wakili
wa serikali, Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Martha Mpazi
kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa ya uchochezi
kinyume na kifungu cha 53(1)(c) na 52(1)(a) cha Sheria ya Habari Namba
12, ya mwaka 2016.
Inadaiwa
mshtakiwa ametenda kosa hilo, Machi 9, mwaka huu akiwa jijini Dar es
Salaam ambapo alitumia mfumo wa kompyuta katika simu yake kupitia
mtandao wake wa Telegram kwa kuandika; “Nimepata wazo kwa group jingine
huko tunaweza kukwepa gharama pia kuandika hata kwenye kuta za wazi
#April 26 Magufuli Out, Pinga Dictator” Maneno ambayo yangeibua chuki
kwa Watanzania.
Mshtakiwa
amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa na
wadhamini wawili watakaosani bondi ya Sh milioni tano. Kesi hiyo
imeahirishwa hadi Mei 24, mwaka huu.
0 comments:
Chapisha Maoni