Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ambaye tangu
juzi yupo uraiani baada ya kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais John
Magufuli, amesema ataanza kushiriki vikao vya Bunge la bajeti mjini
Dodoma baada ya kujua maendeleo ya afya ya mama yake mzazi.
“Nasubiri
ripoti ya daktari kuhusu hali ya mama ndipo niweze kwenda bungeni.
Ripoti hiyo huenda ikatolewa Jumapili (kesho),” amesema Sugu ambaye
alikuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano jela pamoja na na Katibu wa
Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga
Bunge la bajeti lilianza Aprili 3, 2018 na linatarajiwa kumalizika Juni 30,
Sugu
na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela
Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya
fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara
walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini
Mbeya.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.
0 comments:
Chapisha Maoni