Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema yuko tayari
kutolewa kafara au kupigwa risasi kwa kuhubiri viwanda kwa kuwa tayari
amefanikiwa kufufua viwanda 18 kati ya 56.
Pia
amesema hana mamlaka ya kufuta baadhi ya viwanda vilivyobinafsishwa kwa
wamiliki walioshindwa kuviendelea hadi hapo atakapopata baraka za
Baraza la Mawaziri.
Mwijage ametoa kauli hiyo jana Mei 11 bungeni wakati akihitimisha bajeti ya wizara yake kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge.
Alisema
kazi aliyopewa kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa ni kuhakikisha viwanda
vyote bila kujali mmiliki binafsi au serikali, vinafanya kazi vizuri
ndiyo maana serikali inatambua mazingira wezeshi.
Amekiri
kuwa ni kweli Tanzania katika takwimu za Benki ya Dunia haiko vizuri
katika muktasari wa mazingira wezeshi ila ipo katika juu ya wastani wa
asilimia 50.
“Sisi
ni wa 137 kati ya nchi 190, lakini tupo juu ya asilimia 50. Sitaki
kujivuna na hiyo nitafuata maelekezo yenu, ndio maana tunakuja bodi
maalumu ambayo hizi taasisi mnazozilalamikia zitaanza kufanya kazi.
“Nimshukuru
shangazi yangu Riziki Lulida (CUF), alisema nisiwe kondoo wa kafara,
lakini hili la viwanda niko tayari kuwa kafara, nitahubiri viwanda
anayetaka kunipiga risasi anipige risasi.
“Lulida
unajua mtoto hakui kwa shangazi yake, nilipoelekezwa suala la viwanda,
vilivyobinasishwa vilikuwa 156, nilifanya tathmini baada ya Rais kule
Tanga aliponiambia namkwaza. Vilivyokuwa vinafanya kazi vizuri vilikuwa
62, vilivyokuwa havifanyi vizuri 56, vilivyokuwa vinasuasua 28,
vilivyouzwa kwa vipuri mfano injini peke yake vilikuwa 10,” alisema.
Alisema baada ya kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kati ya viwanda 56, viwanda 18 vimekarabatiwa na vimeanza kazi.
“Na
35 vilivyobaki nitawasilisha kwa Spika haya ni mambo ya kitaalamu,
vingine havina sifa ya kuitwa viwanda ila kwa mamlaka niliyonayo siwezi
kuvifuta.
“Kwa
mfano eneo la kiwanda cha kuunga trekta hapo Dar es Salaam nimeenda
kufanya kukagua nikakuta wamejenga shopping mall nzuri kabisa inaajiri
watu, inaitwa Quality Center, mimi mall naipenda kwa sababu inazalisha
ajira, mnanishauri nikabomoe shopping mall?.
“Kulikuwa
na viwanda vya kupasua mbao lakini sasa misitu imekwisha, sasa huyu mtu
nimfanyeje nimuue huyo mtu? Vingine mali ya serikali mfano kiwanda cha
maziwa mali ya NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya), kiwanda cha
serikali siwezi kukichukua.
“Nimemwambia
ajenge kiwanda cha dawa. Yupo kwenye mchakato na suala dawa hivi
namaliza kablda ya asubihi, wengine mnasema Mwijage you are not serious
(hauko makini) siwezi kujiua,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni