Ufafanuzi wa kina ni kama ifuatavyo:
a)
Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB inaongozwa na Sheria ya
HESLB (SURA 178) pamoja na Mwongozo unaotaja sifa, vigezo na utaratibu
wa kuwasilisha maombi ya mikopo. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti
ya HESLB (www.heslb.go.tz) na hautaji kigezo cha umiliki wa leseni kama sifa ya kukosa mkopo;
b)
Pamoja na mwongozo huu, HESLB pia imeandaa kitabu kwa lugha nyepesi ya
kiswahili chenye Maswali na Majibu 21 ili kuwawezesha waombaji mikopo
kufahamu sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ukamilifu
na usahihi. Kitabu hiki pia hakijataja umiliki wa leseni kwa mzazi au
mlezi kama sifa ya mwanafunzi kukosa mkopo;
c)
HESLB inaamini umiliki wa leseni ya biashara kwa wazazi ni jambo jema
na linapaswa kupongezwa kwa kuwa linaimarisha mifumo ya utambuzi kwa
wafanyabiashara.
Bodi
ya Mikopo inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wazazi, walezi na
wanafunzi waombaji wa mikopo kusoma kitabu cha mwongozo wa utoaji wa
mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na kitabu chenye maswali 21 ambavyo
vinapatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).
Vitabu hivi ndiyo nyaraka rasmi za HESLB zinazotoa mwongozo kuhusu maombi ya mikopo kwa mwaka 2018/2019.
Aidha,
HESLB inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wanahabari, kusoma
nyaraka hizo na kutumia kalamu na kamera kuwaelimisha waombaji mikopo
kwa usahihi.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
0 comments:
Chapisha Maoni