Wakati
mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na
kusababisha mafuriko, Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja
wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha
zilizokuwa na upepo mkali.
Akizungumza
kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wa April 9 wakati wakiwa
wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya
Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.
Kamanda
Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa
Baraka (2) huku majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni