Siku
moja kabla ya kuanza mitihani ya kidato cha sita, mtahiniwa wa Shule ya
Sekondari Nyakato, Robert Masaba (21) amekufa ikidaiwa kuwa
amejinyonga.
Kwa
mujibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) watahiniwa 87,643
wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7,
2018 hadi Mei 25, 2018.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinadai Masaba amejinyonga usiku wa kuamkia leo
Mei 6, 2018 kwenye mwembe akiwa Shule ya Sekondari Kahororo.
Masaba
na wenzake walihamishiwa shuleni Kahororo zaidi ya mwaka mmoja uliopita
baada ya sekondari ya Nyakato kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
Mkuu wa Shule ya Kahororo, Omary Rugambaki amezungumzia tukio hilo akisema polisi wameshafika kwa uchunguzi.
0 comments:
Chapisha Maoni