Baraza
la Mitihani Tanzania (Necta) limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa
kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema leo Mei 6, 2018 kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.
Dk
Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya ualimu ambao
watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.
"Maandalizi
kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika,
ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu
mitihani hii," amesema Dk Msonde.
0 comments:
Chapisha Maoni