Mbunge
wa Jimbo la Temeke (CUF), Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi
kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathiri utendaji wa
viongozi (Wabunge) waliopatikana kwa chama hicho kwa namna mbalimbali
ikiwepo namna ya utendaji.
Mtolea
amesema kwamba mgogoro wa chama chake wakati mwingine unakuwa
unawanyima fursa wananchi kuweza kufahamu viongozi wao wanafanya kazi
gani kwani mtandao waliokuwa wanautumia kufikisha habari unakuwa
umekatika.
"Mgogoro
wa chama unatuathiri kwa namna mbalimbali. Kwa mfano sisi wabunge
mtandao wa chama unakuwa umekatika. Wananchi wanakuwa
wamekatika/wamegawanyika. Mbunge unakuwa umefanya mambo mengi lakini wa
kuyasemea kwa wanachi anakuwa hayupo kwa kuwa ule mtandao tu ule
mtandao tuliokuwa tunautumia unakuwa umekatika. Kwa sasa mnasimama nyie
wenyewe tofauti na ilivyokuwa awali" Mtolea.
Aidha,
ameongeza kwamba "Kuwepo kwa mgogoro kuwafanya mnakuwa hamfanyi kazi za
chama zaidi ya kushughulikia migogoro inayoendelea".
Mbali
na hayo Kiongozi huyo amesema mgawanyiko ndani ya chama umepelekea
mzigo mkubwa wa ujenzi wa chama umehamia kwa Wabunge ingawa pamoja na
michango ambayo watakuwa wanaichangia bado maendeleo ya chama hayataweza
kwenda kwa kasi kama jinsi ambavyo wangekuwa wanapata ruzuku.
Mgogoro
wa Chama cha Wananchi CUF unasadikika kuanza pale ambapo Mwenyekiti
Prof. Ibrahim Lipumba alipotaka kurejea kwenye nafasi yake ikiwa ni muda
baada ya kujiuzulu kipindi cha Uchaguzi mkuu 2015 kitendo ambacho
kilisababisha wanachama kugawanyika huku upande mmoja ukimuunga mkono
Katibu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad na wengine wakimuunga mkono
Lipumba.
0 comments:
Chapisha Maoni