Gavana
wa Mji Mkuu wa Kenya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amependekeza mwanasaisa
wa upinzani anayekumbwa na utata Miguna Miguna kuwa Naibu Gavana.
Sonko
ametoa tangazo hilo ambalo halikutarajiwa siku ya (jana) Jumatano jioni
kwa njia ya barua kwa Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi, akisema
Miguna Miguna ametimiza matakwa yote yanayohitajika kikatiba.
Barua
hiyo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maoni mengi
kutoka kwa Wakenya, kutokana na kuwa uteuzi wake umekuja wakati ambao
haukutarajiwa kwa kuwa Bw Miguna amekuwa mkosoaji mkuu wa Gavana huyo na
kabla ya uchaguzi kwa kudai Sonko hana sifa zozote za uongozi na hawezi
kuongoza jiji la Nairobi.
Miguna
alitarajiwa kurudi nchini Kenya siku ya jana kutoka Canada baada ya
kutimuliwa na serikali, lakini akaahirisha safari yake akisema kuwa
idara ya uhamiaji huikumpa pasipoti halali jinsi ilivyoagizwa na
mahakama.
Spika
wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amesema Bw. Miguna
atahitajika kutatua masuala kuhusu uraia wake na serikali ya Kenya kabla
ya kuhojiwa na wabunge wa jimbo hilo.
Bw Miguna anahitaji kuidhinishwa na bunge hilo kabla ya kuchukua wadhifa huo.
Hata hivyo Miguna mpaka sasa bado hajazungumzia chochote kuhusu barua hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni