Muigizaji
wa Bongo movie Sabby Angel ameibuka na kumtolea povu zito Staa wa
Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba baada ya kauli tata aliyoitoa kuhusu
warembo wa Bongo.
Sabby
Angel ambaye alishawahi kukiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ali
Kiba siku za nyuma kidogo ameshindwa kuvumilia na kumpa ukweli Staa Huyo
aliyeoa hivi karibuni.
Hivi
karibuni Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ali Kiba alifunguka
kuwa sababu ya yeye kuwaacha warembo wote wa Bongo na kwenda kuoa Kenya
ni kwa sababu wasichana wengi wakibongo wanaendekeza vigodoro na wengi
sio wasomi.
Sabby Angel ameonekana kukasirishwa na kauli hiyo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani na ameandika ujumbe huu:
"Ni jambo la Kheri kwa Ali K kuoa lakini sijapenda comment yake eti kusema eti Tanzania hakuna wanawake wasomi wa kuoa.
"Binafsi
kama mtu umeamua kuoa we oa tu kwa manufaa yako lakini sio kukashifu
wanawake wote. Kwani hapo wakati anatoka na hao wanawake wa Kitanzania
haukuona hayo mapungufu? Kwani watu wanaoa vyeti? Wanaoa kukimu mahitaji
yao binafsi na kuzaana?.
"Hiyo ni kumaanisha hata wazazi wetu wa kike na hata mama yake ni wale wale it is very immature”.
Ali Kiba alifunga ndoa na binti kutoka Mombasa Kenya wiki chache zilizopita.
0 comments:
Chapisha Maoni