Na.Mwandishi wetu- MAELEZO,Morogoro.
Watumishi
wa Serikali katika Sekta ya Afya, wametakiwa kuwa wazalendo katika
kusimamia fedha za umma ili lengo la kufikisha huduma bora, kwa ukaribu
na kwa wakati kwa wananchi litime kama ilivyo adhma ya serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.
Wito
huo umetolewa jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford
Tandari alipokuwa akifungua mafunzo ya ugatuaji wa mipango ya afya na
bajeti kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya
kutolea huduma(DHFF), kwa wadau wa afya kutoka Mikoa ya
Arusha,Singida,Morogoro,Dodoma,Tanga,Kilimanjaro na Manyara.
‘’Suala
la uwajibikaji katika serikali ya awamu ya tano halina mjadala,
mheshimiwa Rais alipoona mambo hayaendi sawa na kuna mkwamo mahala
Fulani akaamua kutoa maelekezo ya kupeleka fedha moja kwa moja kwenye
vituo vya kutolea huduma, sasa nyinyi kama wasimamizi wa mchakato huo
nivyema mkafanya kila liwezekanalo kuona ni jinsi gani mnasimamia fedha
zinazotolewa na serikali na wafadhili ili zitumike tu kwa lengo
lililokusudiwa tu” Alisema Bw.Tandari.
Alisema
kipindi cha kufanya kazi kwa mazoea sasa kimekwisha na badala yake
watumishi wajipange kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya
tano,akitolea mfano falsafa ya wajapani ya ‘mutos spirit’ yaani kuongeza
uwajibikaji na kufanya kazi za umma kama zakwako binafsi ili kuongeza
ufanisi na matokeo chanya katika kila kazi inayofanyika.
“Mheshimiwa
Rais anaongoza kwa mutos spirit ndio maana anafanyakazi kwa bidii na
maarifa bila kuchoka wala bila kuwa na mawazo ya kwamba atashindwa hii
na sisi watendaji tulio chini yake tuige, kwani wenzetu wameweza wana
nini? Tujitahidi ndugu zangu kufanya kazi kwa kujituma na kwa uadilifu
mkubwa ili basi na sisi baada ya muda mfupi tuonekane kuwa taifa lenye
watu wachapakazi lakini pia wenye maendeleo’’ Alisisitiza.
Mpango
wa ugatuaji wa madaraka ya uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi za
vituo unalenga kupunguza urasimu na kuboresha utoaji huduma za afya,
ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya, utaratibu wa kutoa fedha hasa
mfuko wa Afya wa pamoja (Health Basket Fund) na mfuko wa malipo kwa
ufanisi (Result based Financing) unaozingatia viashiria vya ufanisi
vinavyopimika.
Kwa
upande wake Dkt.Gemini Mtei ,Mkuu wa timu ya Mifumo ya Fedha kutoka
Mradi wa uimarishaji mifumo ya Sekta za umma(PS3,Public Sector System
strenghterning), amesema mradi huo umesaidia kujenga uwezo wa serikali
katika utekelezwaji wa mpango wa DHFF,CHF iliyoboreshwa pamoja na PV.
Dkt.Mtei
alisema PS3 kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wamefanikiwa kufunga mifumo ya
Mipango,Bajeti na utoaji taarifa ambayo imewezesha huduma kuwafikia
wananchi kwa wakati na pia kwa urahisi kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Mradi
wa PS3 unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la
kimataifa la maendeleo la USAID, yenye lengo la kuisaidia serikali
kutekeleza miradi ya koboresha sekta ya Afya na sekta nyinginezo
kulingana na mahitaji na vipaumbele vya serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni