Wanaume
zaidi ya kumi wameibuka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kulalamika kupokwa watoto, huku mamia ya wanawake wanaodai
kutelekezewa watoto wakiendelea kumiminika kwenye ofisi za mkuu huyo wa
mkoa.
Wanaume
hao ambao wamefika leo Jumanne Machi 10, 2018 wamesema hawashindwi
kulea watoto isipokuwa wake zao wamewapoka kwa madai ya umasikini.
Wamesema kama Makonda ameamua kuwasaidia wanawake basi ajue wapo wanaume wanaolia kunyanyaswa na wake zao.
"Mke
wangu alinikimbia nilipougua miguu kiasi cha kushindwa kutembea,
aliondoka na watoto wangu wote watatu, nimekuwa mtu wa mawazo kiasi cha
kupata vidonda vya tumbo naomba awarudishe," amesema Tito Chemba, mkazi
wa Kijichi jijini Dar es Salaam.
Tito (35), amesema ujio wake kwa Makonda ni kutaka kurejeshewa wanawe wanaoishi Bukoba kwa ndugu wa mkewe.
Mwanamume mwingine, Edmond Mbisho amesema mkewe aliondoka na mtoto wake tangu akiwa na miaka mitatu na sasa ana miaka sita.
“Ninachoomba ni kupata mwanangu si kingine, kwa sasa mwanamke anaishi na mtu mwingine," amesema.
Mwanamume
mwingine, Vedasto Mdesa mkazi wa Iringa amesema watoto wake watatu
waliozaliwa kwa pamoja walichukuliwa na ndugu wa mkewe na kupelekwa
Urusi.
"Nilipokwa
watoto kisa mimi ni masikini, hivi sasa naishi kwa tabu na sababu kubwa
ni umasikini na wanasema sijasoma. Huyo mwanamke ana shahada na mimi ni
mpiga picha nisiye na elimu," amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni