Serikali
imesema kuwa zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali
inapobainika kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye
athari kwa jamii hususani watoto.
Hatua
mojawapo ambazo zitachukiwa na serikali ni pamoja na kutoa onyo,
kufungiwa, kufungiwa kutoa huduma kwa kipindi kitakachotajwa au
kufungiwa kutojihusisha kabisa na utangazaji.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema
hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mororogo
Kusini, Prosper Joseph Mbena aliyehoji kuongezeka kwa matangazo ya
biashara kwenye vyombo vya habari na kwamba baadhi ya matangazo hayo
huwakera na kuleta hisia tofauti kwa baadhi ya watu hasa watoto kutokana
na maudhui mabaya ya baadhi ya matangazo hayo
“Serikali
tayari ina vyombo vya kusimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini
yakiwepo maudhui katika matangazo vyombo hivyo ni mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania(TCRA)ambayo iliundwa na Kamati ya Maudhui ya kifungu namba 26,
Kamati hii inayosimamia maudhui na matangazo ya Kielekronic yaani
redioni na Televisheni pamoja na mitandao ya kijamii,” amesema Shonza.
“Chombo
cha pili ni bodi ya Filamu Tanzania ambayo inasimamia maudhui katika
picha jengezi zinazoonyeshwa katika jumba la sinema, hadharani vilevile
katika michezo ya kuigiza
"
Idara ya Habari Maelezo ni chombo cha tatu ambayo imewekwa chini ya
kifungu cha sheria namba nne kifungu cha sheria ya habari namba 12 ya
mwaka 2016 kinachosimamia maudhui katika machapishombalimbali yakiwemo
magazeti, majarida pamoja na vipeperushi,” ameongeza.
“Zipo
hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika bila kutia
shaka kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari
kwa jamii
"
Hatua hizo ni pamoja na kutoa onyo, kufungiwa, kufungiwa kutoa huduma
kwa kipindi kitakachotajwa au kufungiwa kutojihusisha kabisa na
utangazaji au uchapishaji wa habari pamoja na matangazo.
"Serikali inaendelea kuhimiza jamii nzima kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika kusambaza habari mbalimbali kwa jamii.”
0 comments:
Chapisha Maoni