Mfanyakazi
wa Shirika la Umeme (Tanesco) Kibaha, Chande Kipae, amefariki dunia
baada ya kunaswa na umeme wakati akiondoa nyaya za umeme zilizokuwa
zimekatika.
Tukio
hilo limetokea April 16 saa tisa jioni wakati Chande akiwa na mtoto
wake Jumanne Chande wakielekea mjini kutafuta mahitaji ya familia.
Uongozi
wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi umethibitisha kupokea
mwili wa marehemu huyo na kwamba waliufanyia uchunguzi na kukabidhi kwa
ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Taarifa
kutoka Shirika la Umeme Tanesco Mkoani Pwani, Madulu zilithibitisha
kutokea kwa kifo cha mfanyakazi huyo huku ikidaiwa kwamba siku ya tukio
aliomba ruhusa ofisini kwa ajili ya masuala yake binafsi.
0 comments:
Chapisha Maoni