Viongozi
wawili wa Baraza la la Wazee Taifa la CHADEMA, wanashikiliwa na Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo Aprili 17, 2018 ambapo
mpaka sasa haijafahamika kusudio la kukamatwa kwao.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje
Chadema, John Mrema wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari
hizi na kuwataja viongozi hao waliokamatwa kuwa ni dereva Proaches
Urassa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Jimbo la Morogoro Kusini Mzee
Daniel Banzi.
"Jambo
la kusikitisha ni kuwa jana usiku Polisi walivamia walikokuwa wamelala
Viongozi na kuwakamata baadhi yao ambao walikuwa kwenye ziara ya
kukutana na wazee kwenye vikao vya ndani.
"Hakuna
maelezo ya maana yanayotolewa zaidi ya Polisi kusema ni ukaguzi wa
kawaida, ila ukweli ni kwamba kila wanapoonekana viongozi wa CHADEMA
Polisi wanawakamata", amesema Mrema.
Pamoja
na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "mpaka sasa tumewatuma Mawakili
wetu mkoani Morogoro ili waweze kujua viongozi hao walikamatwa kutokana
na tatizo gani. Tunalaani kwa nguvu zote udhalilishaji huu unaofanywa
dhidi ya viongozi na wanachama wetu".


0 comments:
Chapisha Maoni