Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ametuma salamu za rambi
rambi kwa wanachama wa Chadema baada ya kuondokewa na kiongozi wake
mkubwa, Philemon Ndesamburo.
Pia Zitto amempa pole, mtoto wa marehemu Ndesamburo, Lucy Owenya kwa kumpoteza baba yake.
Zitto
ameandika katika ukurasa wake wa Facebook leo na kusema; “Ni msiba
mkubwa kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa
Pesa alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka
2015. Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake
mbele kuliko kitu kingine chochote.”
Zitto
amesema msiba wa Ndesamburo ni mkubwa kwa wanaChadema ambacho alikuwa
Mwenyekiti wake wa Mkoa tangu chama kimeanzishwa mpaka mauti
yalipomkuta.
“Huwezi
kutaja maendeleo ya Chadema kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la mzee
Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi kwa karibu, naweza
kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda chama chake
kwa dhati kabisa,” amesema
Kadhalika
Zitto anaendelea kummwagia sifa Ndesamburo akisema Tanzania ina faidi
matunda ya vyama vingi kwa sababu ya kazi kubwa aliyofanya Mzee
Ndesamburo.
“Nawapa
pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya Mzee Ndesamburo. Mzee wetu
aliishi maisha yake na ameacha ' legacy ' yake. Najua maumivu yenu
lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye mtihani huu
mkubwa. muwe wamoja na mshikamane.” Amesema na kuongeza:
“Poleni
sana ndugu zangu wa Chadema kwa kupotelewa na kiongozi wenu na kiongozi
wetu pia. Poleni sana wana Moshi Mjini na wana Kilimanjaro wote.
Poleni Sana Watanzania.pumzika kwa Amani Philemon Kiwelu Ndesamburo.
Hiyo ni njia yetu sote. Amina.”
0 comments:
Chapisha Maoni