Ikiwa
ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Haule
Filikunjombe afariki dunia, mke wa wake Sarah Habiba amesema Tanzania
ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo.
Kwenye
ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, huku
wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu.
"Mume
wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli
umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto
wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi
wangu, ntakukumbuka daima mpenzi", aliandika jana Sarah Habiba.
Deo
Filikunjombe alifariki Octoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta
iliyoanguka kwenye msitu wa hifadhi ya Selous akitokea Dar es salaam
kwenda Ludewa, akiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi
wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera ambao pia
walifariki dunia.
Deo
Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha
kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa na wabunge wengine,
akiwemo rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
0 comments:
Chapisha Maoni