Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la
Kifalme la Buckingham Palace.
Makamu
wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake
katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa
ikichukua hatua mbali mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado
hatujawa na tekinolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote
lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.
Kwa
upande wake Prince Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika
kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu
na pia Prince William amemualika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya
Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.


0 comments:
Chapisha Maoni