Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George
Mkuchika amefunguka na kumpongeza Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya
ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe kwa kuendelea kumpigania diwani wa CCM
Simon Kanguye ambaye amepotea kwa kutekwa toka mwaka jana.
Zitto Kabwe alihoji bungeni juu ya kupotea kwa Simon Kanguye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo ambaye anadaiwa kutekwa miezi 9 sasa na hafahamiki wapi yupo hivyo alihitaji vyombo vya usalama viweze kuweka wazi jambo hilo ili wajue kama ameshakufa ili waweke matanga au kama wao wanamshikilia.
Kufuatia
taarifa hiyo serikali kupitia kwa Waziri Mkuchika ndipo ikaweka wazi
kuwa jambo hilo lipo chini ya jeshi la polisi lakini alitumia nafasi
hiyo kumpongeza Zitto Kabwe kwa kuweza kufuatilia jambo hilo ili hali
diwani huyo ni mwanachana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Navyomuelewa
Zitto Kabwe alivyo msomi, kijana anayeipenda nchi yake tena ana akili
simuoni Zitto anahamasisha watu kuchukua sheria mkononi bali yale maneno
aliyaweka tu kutuhimiza watu wa serikali jamanii eehh fanyieni kazi, na
sisi tumelipokea.
"
Ila suala la kupotea kwa diwani huyo lilisharipotiwa polisi na
uchunguzi unaendelea na tena hapa nampongeza ndugu yangu Zitto Kabwe,
huyu diwani anayemtetea tumtafute mpaka tumpate wala siyo wa chama chake
cha ACT Wazalendo bali ni diwani wa CCM.
"
Hii inaonyesha jinsi alivyomzalendo, anavyopenda haki itendeke kwa kila
mtu... sasa uendelee hivyo hivyo mdogo wangu Zitto usiyumbe kwenye
mengine endelea hivyo hivyo" alisisitiza Mkuchika


0 comments:
Chapisha Maoni