Kamati
ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) iliyoundwa kujadili uamuzi
wa Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali (AG)wa kuzifanyia mabadiliko kanuni
za uchaguzi wa chama hicho imesema, AG hakuwa na mamlaka ya kufanya
mabadiliko yoyote.
Hayo yameibuka leo Aprili 14 wakati wa uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa chama hicho, mjini Arusha.
Katika
tukio hilo, Makamu wa Rais wa sasa wa TLS, Godwin Ngwilimi, ametoa
hoja hiyo na kumtaka mjumbe wa Baraza la uongozi, Jeremiah Mtobesya
kusoma mapendekezo hayo ambayo yalisema Mwanasheria Mkuu wa serikali
hakuwa na Mamlaka ya kufanya mabadiliko bali kuyachapisha kwenye gazeti
la serikali.
Pia
walipendekeza kufuata njia za kiutawala kuonana na Mwanasheria Mkuu au
kwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya mamlaka yake kwa TLS.
Mgombea
Urais wa TLS, Fatma Karume amesema maboresho yaliyofanywa hayana msingi
wa kisheria kwa kuwa kanuni za uchaguzi wa TLS zinaanza kufanya kazi
mara tu baada ya kupitishwa na mkutano mkuu.
Hata
hivyo wajumbe hao walikubaliana na baraza la uongozi kutengeneza kanuni
ambazo zitatamka kuwa si lazima zitangazwe kwenye gazeti la serikali
ili ziwe halali.


0 comments:
Chapisha Maoni