Hisia
mbalimbali zimejitokeza duniani ikiwa baadhi ya watu wanaunga mkono
mashambulizi hayo na wengine kukosoa shambulizi hilo la anga
lililofanywa mapema Jumamosi na majeshi ya Marekani, Ufaransa na
Uingereza dhidi ya vituo vya serikali ya Syria.
Lakini hali ni tofauti kidogo Syria ambapo Mamia
ya wananchi wa Syria wamejitokeza katika mji mkuu wa Damascus, Jumamosi
hii wakiendesha magari huku honi zikilia, wakionyesha alama ya ushindi na
kupeperusha bendera za Syria kwa kupinga mashambulizi ya kijeshi ya
pamoja yaliyofanywa na nchi hizo tatu. Wengine walikuwa wakipiga
makelele wakisema, "Sisi ni watu wako, Bashar."
Ndege
za kivita za nchi za Ulaya na manuari za kijeshi zilishambulia kwa
makombora vituo vitatu vya silaha za kemikali nchini Syria, shambulizi
la awali ambalo linaweza kugeuka kuwa ni muendelezo wa kampeni ya
kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al- Assad na wanao muunga
mkono.
Washirika
wa Syria, ikiwemo Urusi wamesema kuwa shambulizi hilo la pamoja dhidi
ya Syria limefeli. Wizara ya mambo ya nje imesema idadi kubwa ya
makombora yaliyopigwa Syria yaliangamizwa na mfumo ya ulinzi wa serikali
ya Syria.
Katika
mkutano wa waandishi wa habari London Jumamosi, Waziri Mkuu wa
Uingereza Theresa May amesema nia ya kuratibu mashambulizi haya sio kwa
ajili ya “kuipindua serikali,” lakini ni “kupunguza na kuzuia” uwezo wa
serikali ya Assad kutumia silaha za kemikali.
Ameongeza
kuwa jumuiya ya kimataifa haiwezi kusimama kando na “kutupia macho tu”
wakati utawala wa Syria ukiendelea kutumia silaha za kemikali dhidi ya
watu wake.
Huko
Paris, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa tamko akisema, “
Hatuwezi kuvumilia kitendo cha kufanya matumizi ya silaha za nyuklia ni
mwenendo wa kawaida,” akiongeza kuwa “ukweli wa taarifa na kuhusika kwa
utawala wa Syria hauna mashaka.
Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel amesema anaunga mkono mashambulizi ya
kijeshi yaliyofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza.
Amesema mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa yanapaswa kuwa onyo kwa utawala wa Syria kutoendelea kutumia silaha za sumu.
Wakati
huohuo Serikali ya Iran imesema imesema kuwa Marekani, Ufaransa na
Uingereza hazitaweza kupata manufaa yoyote kwa kuishambulia Syria.



0 comments:
Chapisha Maoni