Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema
inaudhi kuona msanii wa filamu, Amri Athuman maarufu King Majuto anaomba
msaada wa Sh 500,000 kwa ajili ya matibabu wakati kuna makampuni
yalifaidika naye kwa kuingia mikataba aliyodai ya dhuluma.
Kutokana
na hali hiyo, amesema serikali imechoka kusikia vilio vya wasanii wa
filamu kudhulumiwa haki zao na sasa imeunda kamati maalumu ya wanasheria
kukagua mikataba yote ya mashirika na makampuni waliyoingia wasanii
akiwamo King Majuto na marehemu Seteven Kanumba ‘Kanumba’.
Pia
imeagiza wasanii wote ambao wanaona wameingia mikataba ya kipumbavu na
makampuni au mashirika hayo wawasilishe taarifa zao kwa serikali.
Dk.
Mwakyembe amesema hayo jana Aprili 27, bungeni jijini Dodoma wakati
akijibu hoja za wabunge katika kuhitimisha hotuba ya bajeti ya wizara
hiyo.
“Kwa
kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’
(watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana Watanzania wetu. Hili
limeanza kubadilika tumeanza kuwa- empower (kuwezesha) wasanii wetu kwa
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wasitumie middle
men.
“Kwa
mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua
ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri
mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu,”
alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema
licha ya kwamba nusu ya mabango ya biashara na matangazo ya biashara ni
ya Mzee Majuto inashangaza kuona anaomba fedha ya matibabu.
0 comments:
Chapisha Maoni