Mkutano
wa kihistoria baina ya Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na Rais
wa Korea Kusini Moon Jae-in umeanza Ijumaa kaitka kijiji cha truce
village huko Panmunjom.
Kim
Jong-un alivuka eneo la mpakani lisilokuwa na harakati za kijeshi
ambalo limeyagawanya mataifa hayo mawili kwa zaidi ya miaka 60.
Hatimaye
viongozi hao kutoka upande wa utawala wa kikomunisti (kaskazini) na
upande wa utawala wa kidemokrasia (kusini) walikaribiana kabla ya
kutangaza azma yao ya kuondoa silaha za nyuklia na kuendeleza amani.
“Leo,
Mwenyikiti Kim Jong Un na mimi tumethibitisha ile azma yetu ya kufikia
hali ya kutokuwepo silaha za nyuklia katika eneo la rasi ya Korea katika
hatua ya kuondosha kabisa silaha za nyuklia ikiwa ni lengo letu la
pamoja,” amesema Rais Moon Jae katika sherehe za kutangaza makubaliano
ambayo wameyaita tamko la Panmunjom.
Kiongozi
wa Korea Kaskazini kwa upande wake amesema kuwa amekubaliana na Tangazo
hilo la pamoja na mikataba iliyotangulia baina ya nchi hizo mbili bila
ya kufafanua au kuthibitisha matokeo ya makubaliano hayo ya kuondosha
vitisho vya programu ya silaha za nyuklia za nchi hiyo
“Tumeamua
kufungua awamu hii ya kuboresha mahusiano na maendeleo kwa kutekeleza
kikamilifu Tangazo la Kaskazini- Kusini na mikataba yote iliyotangulia
ambayo ilikubalika.,” amesema Kim.
0 comments:
Chapisha Maoni