Rais
wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye, amehukumiwa miaka 24 jela
baada ya kukutwa na hatia katika matumizi mabaya ya madaraka na
kusababisha nchi kushuka kiuchumi.
Park
Geun-hye aliondolewa madarakani mwaka jana baada ya kutuhumiwa kutumia
vibaya wadhifa wake na kusababisha kuanguka kwa uchumi.
Rafiki
yake Choi Soon-sil, anayehusishwa na kashfa hiyo, alihukumiwa wiki
mbili zilizopita hadi miaka 20 jela kwa kupokea hongo iliyotolewa na
makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na makampuni yai Samsung na
Lotte.
Katika
mashtaka yake, mwendesha mashtaka alimshtaki rais wa zamani kuwa
“alisababisha mgogoro wa kitaifa kwa kuacha mtu ambaye hajawahi
kushiriki katika usimamizi wa umma kuongoza nchi”.
0 comments:
Chapisha Maoni