Aliyekuwa
rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefikishwa mahakamani leo katika mji
wa Durban ili kujibu mashtaka ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha
kinyume cha sheria.
Kesi hii inasikilizwa kwa mara ya kwanza na inahusu biashara ya zamani ya mauzo ya silaha tangu miaka ya 1990.
Rais
wa zamani wa Afrika Kusini anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa
Thomson CSF – jina la zamani la kampuni ya Thales – katika mpango wa
mkataba wa mauzo ya silaha wenye thamani ya karibu Euro Bilioni 4
ulioafikiwa mnamo mwaka 1999.
Wakati
huo, Jacob Zuma alikua makamu wa rais wa nchi ya Afrika Kusini.
Anashutumiwa kuwa alipokea jumla ya euro milioni 50 kutoka kampuni ya
Ufaransa ya Thales. Kwa upande mwingine, aliahidi kupitishia zabuni
kampuni hiyo ya Thales.
Kwa
jumla, Afrika Kusini iliamua kutumia zaidi ya dola bilioni 10 kurejelea
upya silaha zake. Silaha ambazo nchi hiyo haikuweza kuzihitaji wakati
huo na ambazo hazitumiwi leo. Lakini sababu kuu ni kwamba zaidi ya dola
milioni 300 (hongo) zililipwa wakati wa mikataba hii.
0 comments:
Chapisha Maoni