Msanii
Roma Mkatoliki ametimiza masharti aliyopewa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kumtaka ajisajili
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kuwa akifanya hivyo atakuwa
ametambulika na kuwa huru kufanya kazi.
Roma
Mkatoliki jana April 5, 2018 amekwenda Baraza la Sanaa la Taifa na
kujisajili kama ambavyo aliagizwa na viongozi wa serikali na kusema
kuanzia leo atakuwa huru kufanya kazi na sasa anarudi rasmi katika
muziki.
Mar
1, 2018 Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki alifungiwa
kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa
msanii huyo kudharau wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msanii huyo ametumikia kifungo hicho kwa mwezi mmoja na siku tano hivyo kifungo chake kimeisha jana baada ya kujisajili BASATA.
Msanii
Roma Mkatoliki ajisajili na kukabidhiwa rasmi cheti cha kutambulika na
Baraza la sanaa la Taifa jana April 05 2018, Hii ni baada ya kupewa
sharti na Wizara ya Habari ya kujisajili kwanza Basata ili aondolewe
adhabu yake ya kufungiwa miezi 6.
0 comments:
Chapisha Maoni