Waziri
wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia
ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na
chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.
Ndalicho ameyasema hayo leo Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.
Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.
“Serikali
ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona
kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripoti ya CAG, inatupa chachu ya
kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,”
amesema
Amesema
kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia
watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma.
Ndalichako
alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano
iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa madeni hayo.
“Taarifa
ya CAG 2015/16 hadi 2016/17 inaionyesha kuwa makusanyo yameongezeka
kutoka Sh28bilioni hadi Sh 116bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia 300.
Takwimu hazidanganyi,” amesema
Hata
hivyo amesema bado makusanyo hayo hayatoshelezi na ameitaka
Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kuhakikisha ukusanyaji wa mikopo
unaimarishwa.


0 comments:
Chapisha Maoni