Kamati
ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeiagiza Serikali kupiga
marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi ili
kulinusuru Taifa na madhara yanayotokana na mifuko hiyo.
Maagizo
hayo yalitolewa baada ya kamati hiyo jana kukutana na Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira na Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji.
Akizungumza
jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadiq Murad alisema walipata maelezo
kutoka serikalini kuwa uzalishaji katika viwanda 41 vya plastiki nchini
ulikuwa ni tani 73 katika mwaka 2016.
Hata hivyo, alisema mifuko iliyoingia nchini kupitia bandarini na mipakani ilikuwa tani 1,375.
“Kamati ilishauri ipigwe marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi na iwekwe tahadhari katika mipaka yetu,” alisema.
Alisema
kamati inaitaka Serikali kufanya uhakiki wa uzalishaji katika viwanda
vya nchini ambavyo vimepunguza uzalishaji ili waweze kukaa chini na
kuzalisha mifuko ambayo itakayokidhi mahitaji na vigezo.
“Na
hii itakuwa ni ya muda kuzalisha mifuko hiyo kwa masharti ya vigezo
baadaye Tanzania isiwe na uzalishaji wa mifuko hii tena inayoharibu
mazingira,” alisema.
Murad
alisema zipo nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, Uganda na Zanzibar
ambazo zimepiga marufuku uzalishaji na uingizaji wa mifuko hiyo na
kutafuta mifuko mingine inayotengenezwa na nguo, karatasi na majani.
Alisema
mfano mzuri ni Zanzibar ambayo imepiga marufuku mifuko hiyo tangu mwaka
2016 na mtu anapoingia na mifuko hiyo bandarini hunyang’anywa na kupewa
mingine.
“Tueleweke
kabisa sisi kama kamati hatutaki kiwanda chochote kifungwe, tunataka
uzalishaji kwa kufuata masharti na vigezo. Tunaunga mkono juhudi za Rais
John Magufuli za kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda lakini vigezo
na masharti lazima yazingatiwe,” alisema.
Akizungumzia
agizo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January
Makamba alisema hawaja japelekewa rasmi hayo mapendekezo. Hata hivyo
alisema watapiga marufuku mifuko yote ya ndani na nje. “Wenye viwanda
wajiandae maana yake dhamira ya Serikali wanaijua tangu mwaka 2016,”
alisema
0 comments:
Chapisha Maoni