Winnie
Madikizela Mandela, amezikwa Jumamosi jioni kando ya wajukuu wake
wawili katika kaburi la familia lililo kwenye kitongoji cha Fourways,
takriban kilomita 40 Kaskazini mwa mji wa Soweto, Afrika Kusini.
Bi
Mandela, ambaye alikuwa mmoja wa mashujaa waliopambana kidete na
ubaguzi wa rangi na ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mke wa zamani wa
rais wa kwanza wa nchi hiyo, Nelson Mandela, aliaga dunia tarehe mbili
mwezi huu.
Leo
Jumamosi, maelfu ya wambolezaji walikusanyika katika uwanja wa Orlando,
ulio mjini Soweto, kutoa heshima zao za mwisho katika hafla ambayo
ilitajwa na shirika la habari la Reuters kama iliyoiunganisha mirengo
yote ya kisiasa nchini humo.
Shirika hilo liliripoti kwamba marais wawili wa zamani wanchi hiyo, Thambo Mbeki na Jacob Zuma, pia wamehudhuria mazishi hayo.
Bintiye
Winnie, Zenani Mandela-Dlamini, ni kati ya waliotoa hotuba wakati wa
maziko hayo. Viongozi waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na marais wa
Jamhuri ya Congo, Namibia, na wanaharakati wa haki za raia kutoka
ulimwenguni kote, akiwemo Mchungaji Jesse Jackson kutoka Marekani.
Aidha
mazishi hayo yamehuduriwa na waombolezaji kutoka maeneo nchi mbalimbali
ulimwenguni kote. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alikuwa wa
kwanza kutupa mchanga kwenye kaburi la Winnie Mandela.
Jeneza
la Winnie lilifunikwa na bendera ya Afrika Kusini, huku baadhi ya
waombolezaji wakivalia nguo zenye rangi ya chama cha African National
Congress (ANC).
Mazishi
hayo yalihitimisha siku 10 za maombolezo ya kitaifa, kipindi ambacho
kiliwapa fursa maelfu ya watu kutoa heshima zao za mwisho nyumani kwa
Winnie, ambaye alifahamika na wengi kama Mama wa taifa.






0 comments:
Chapisha Maoni