Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema matatizo ya wanandoa
hayatakiwi kumuathiri mtoto kiasi cha kumnyima haki zake.
Amesema,
hata kama mtoto amezaliwa nje ya ndoa, ana haki sawa na ndiyo maana
sheria ya mtoto (ya mwaka 2009) haijasema ni mtoto yupi, bali inamgusa
kila mtoto.
“Haijalishi mtoto amezaliwa na ‘house girl, sheria haibagui mtoto inawalinda watoto wote,” amesema
Ameyasema hayo leo Aprili 14, katika mahojiano maalumu yanayorushwa mubashara na televisheni ya TBC.
“Ajenda kuu tunayoizingatia ni haki ya mtoto. Watoto wote wa ndani na nje ya ndoa wana haki sawa,” amesema.
Kadhalika,
amewataka viongozi wa dini kutoa mafunzo ya malezi na wajibu wa wazazi
kwa watoto kabla ya kufikia hatua ya kufunga ndoa.
“Mapungufu
yaliyopo katika sheria yanawafanya maofisa wa ustawi wa jamii waonekane
hawafanyi kazi. Mapungufu haya ya kisheria yanawanyima kufanya kazi kwa
ufanisi.” Amesema


0 comments:
Chapisha Maoni