Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Rayc
amewatolea povu zito watu wote ambao waliowahi kumsema kuhusu ubonge
wake siku za nyuma.
Rayc
ni moja kati ya wasanii wa kike ambao miaka kama kumi iliyopita enzi za
ustaa wake alikuwa anavutia sana hadi kufikia hatua ya kuitwa kiuno
bila mfupa.
Lakini
alinenepa sana miaka ya hivi karibuni baada ya kuacha kutumia madawa ya
kulevya kupelekea watu kumkejeli alipokuwa anashindwa kukata mauno kama
zamani kutokana na mwili mkubwa.
Lakini
saivi Rayc amepunguza kilo nyingi tu na kupitia ukurasa wake wa
Instagram ameweka picha yake inayomuonyesha akiwa mwembamba kupita kiasi
ambapo ameweka picha hiyo na kusindika kwa maneno haya: Wale wote walionikejeli nilivyonenepa mat.. yenu!”.



0 comments:
Chapisha Maoni