Upande
wa Jamhuri katika kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania
(TSNP), Abdul Nondo, Veronica Fredy anatarajiwa kuletwa makamani kutoa
ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.
Mbali
na mpenzi huyo wa Nondo, Jamhuri pia inakusudia kuleta mashahidi
wengine wanne ambao ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir
na mfanyakazi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.
Kesi
hiyo ilikuja leo mbele ya hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa, John
Mpitanjia kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo Wakili wa
Serikali, Abel Mwandalamo amesema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili
ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijini Dar Es Salaam
na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo
cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Wakili
Mwandalamo amedai upande wa Jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo
vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya
simu, maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta
kielelezo cha simu za mkononi.
Hakimu
Mpita Njia ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, mwaka huu ambapo
itaanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, kutokana na maombi ya
upande wa utetezi ya Wakili Charles Luoga.
0 comments:
Chapisha Maoni