Tangu jana wanawake waliotelekezwa na waume zao wamefika katika ofisi hizo zilizopo Ilala jijini hapa, kuanza kusikilizwa.
Katika
ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akijibu
maoni ya wachangiaji, Dk Ndugulile alivionya vyombo vya habari kwa
kushiriki kuonyesha picha za watoto katika mikusanyiko hiyo, huku
akitaka utaratibu ufuatwe katika kusikiliza mashauri ya walalamikaji
ikiwa ni pamoja na usiri.
“Ni
kosa kisheria kwa chombo cha habari au mitandao ya jamii kuonyesha
picha zenye kumdhalilisha mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto Namba 21
ya 2009. Navikumbusha vyombo vya habari kulinda haki za watoto na
kutokuwa washirika katika kudhalilisha haki za watoto,” alisema Dk
Ndugulile kupitia ujumbe wa Twitter.
“Ushauri
wangu kama Wizara inayosimamia haki za watoto, suala kama hili
linapaswa kufanyika kwa faragha, kwa sababu una deal na watu na litakuwa
endelevu,” amesema Dk Ndugulile.
“Anachokifanya
Makonda ni jambo zuri, lakini linahitaji uangalifu na tufuate mifumo
sahihi. Nitoe rai kwa wananchi wote kufuata taasisi zinazohusika.”
Alipoulizwa
sababu ya wananchi wengi kujitokeza kwa mkuu wa mkoa kama ishara ya
kuzidiwa kwa idara ya Ustawi wa Jamii, Dk Ndugulile alikanusha ,
“Si
kwamba Ustawi wa Jamii umezidiwa, inawezekana wananchi hawana taarifa
za kutosha kwa hiyo kupitia mikutano kama hiyo watapata taarifa. Tufuate
mifumo rasmi inayokubalika kisheria,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni