Ofisi
ya Uhamiaji Mkoa wa Dar-Es-Salaam, imemwandikia barua Askofu Mkuu wa
Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe,
kumwita kwa ajili ya mahojiano.
Askofu
Kakobe ametakiwa kufika katika ofisi hiyo, Jumatatu 9.4.2018 saa 4
asubuhi, na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ili
kuhojiwa juu ya uraia wake.
Alipoulizwa
kwa njia ya simu, Askofu Kakobe amethibitisha kupokea barua hiyo, na
kusema kifupi tu kwamba, atakwenda kwenye mahojiano hayo.
Tukio
hili linakuja baada ya sekeseke kati ya Askofu huyo na TRA,
kuhitimishwa tarehe 20.2.2018, siku ambayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alipotoa taarifa kwa umma juu ya
uchunguzi wao; na baadaye kusema mjadala huo umefungwa.


0 comments:
Chapisha Maoni