Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutotishwa na maandamano ya mitandaoni
yanayoratibiwa na Mange Kimambi, kwani mkoa wa Arusha uko salama.
Mrisho
Gambo ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa salam zake kwa Rais Magufuli,
kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba za polisi mkoani Arusha, kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abedi.
Kwenye
salamu hizo Mrisho Gambo amesema mkoa wa Arusha ni salama na wakazi wa
Arusha hawana haja ya maandamano, kwani wanachohitaji ni uongozi wake
ambao unawaletea maendeleo makubwa.
Mrisho
gambo aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua kazi ya kubwa aliyonayo
Rais ya kupigana vita ya uchumi, na watu wengi wasiopenda nchi hii
watachukia kutokana na hilo.
“Mheshimiwa
Rais nikuhakikishie tu Arusha ni salama, wala usitishwe na mbwembwe za
kwenye mitandao, watanzania halisi ni hawa hapa wenye Arusha yao.
"Watanzania
wa Arusha wamechoka na maandamano, wanataka uongozi wa kwako ambao
unawaletea maendeleo. Ninajua vita uliyokuwa nayo ni kubwa sana, Mwl.
Nyerere alikuwa na vita ya ukombozi, akaimaliza salama,
"Mheshimiwa
Rais vita yako wewe ni ya kiuchumi, ni vita inayopigana na mabeberu
ambao wanawatumia wengine kukwamisha jitihada zako. Watu wengi ambao
hawaitakii mema nchi hii hawawezi kuipenda”, amesema Mrisho Gambo.
Sambamba
na hilo Mkuu wa mkoa huyo wa Arusha amemshukuru Rais Magufuli na wadau
kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo za askari polisi, ambazo awali
ziliteketea kwa moto.


0 comments:
Chapisha Maoni