Ikulu
ya Marekani, White House imetangaza vikwazo dhidi ya Warusi 38 na
makampuni, ikisema Marekani inakabiliana na kile kinachoendelea ikiwa ni
mbinu za Serikali ya Urusi za “vitendo vya kuvuruga” demokrasia nchi
za Magharibi na ulimwenguni kote.
Katika
muhtasari alioutoa msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders Ijumaa
amesema Marekani bado inataka kushirikiana naUrusi
“Pia,
kile tunachotaka kukiona ni serikali ya Urusi ibadilishe mwenendo wake
kikamilifu. Tunataka kuendelea kuwa na mazungumzo na kufanya kazi siku
za usoni kwa kujenga mahusiano mazuri,” Sanders amesema.
Vikwazo
hivyo vitawekwa dhidi ya makampuni saba ya Urusi – ikiwemo Oleg
Deripaska, kampuni ya aluminium ambayo ni mshirika wa karibu na Rais
Vladimir Putin- na makampuni mengine 12 ambayo wanayamiliki au
kuyahodhi.
Pia
maafisa 17 wa serikali ya Urusi, na kampuni ya kutengeneza silaha
inayomilikiwa na serikali ya Urusi na kampuni zake tanzu, benki ya
Urusi, pia zitalengwa na vikwazo hivyo.


0 comments:
Chapisha Maoni