Mbunge
wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hillary (CCM), ameeleza kushangazwa na
kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni 15 kati ya Sh bilioni 80
zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na kwamba iwapo
serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana
mashati bungeni.
Akichangia
hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini
Dodoma jana Ijumaa aprili 6, Aesh alisema fedha hizo zilizotengwa
zinatosha kunua mahindi Wilaya ya Sumbawanga pekee.
“Kama
mkishindwa kununua haya mahindi msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga
mkaja kufungua wakati muda umekwenda na kuweka masharti magumu,
nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka tutashikana
mashati humu ndani.
“Siyo
kazi ya mkulima kuhakikisha nchi haina njaa ni kazi ya Serikali,
nashangaa huku mnasema tu tumbaku na pamba, bila mahindi huyo mkulima
hawezi kulima hayo mazao yake,” alisema Aesh.
Aeshi
pia amezungumzia watumishi wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi
akisema mmoja wa Madereva waliofukuzwa kazi alimwendesha mpaka Waziri
Mkuu Mstaafu (hakutaja jina la waziri huyo).
“Huyu
dereva alikuwa amebakisha miaka mitano tu astaafu, sasa hivi mmemfukuza
kazi hana cha kufanya, suala hili mliangalie upya,” alisema.


0 comments:
Chapisha Maoni