Muigizaji
wa Bongo movie Salma Jabu 'Nisha' anayefanya vizuri hivi sasa na
ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya
kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.
Siku
ya Alhamis msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema
kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha
alikuwa anamtongoza Young Dee.
Amber
Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana
ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku akikiri kuwa Nisha ni
fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.
Baada
ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya
kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi
kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:
"Mimi
sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka
kuingia kwenye muziki hivyo Young Dee kama msanii wa Bongo fleva
alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.
"
Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber
Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu
nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.


0 comments:
Chapisha Maoni