Polisi
mkoani Shinyanga wanamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 90, Kachuka
Malongo kwa tuhuma za kubaka wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Tinde,
Wilaya ya Shinyanga.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,
ACP Simon Haule alisema kwamba wanafunzi hao walibakwa kwa nyakati
tofauti na mtuhumiwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa.
“Tumebaini
chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa na uchu wa mapenzi. Tayari
tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika
tutampeleka mahakamani,” alisema Kamanda Haule.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda Haule alisema kwamba mkazi wa Tinde, Amada Mganyizi
ndiye aliyebaini kubakwa kwa wanafunzi hao Machi 21 saa 2:30 asubuhi.
Hata hivyo, hakueleza kwa undani namna gani mkazi huyo alibaini kubakwa
kwa watoto hao.
Alisema
kwamba wanafunzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa wana umri wa kati
ya miaka minane na 12 na wanasoma katika shule za msingi Tinde A na B.
“Natoa
rai kwa wananchi na wazazi kuwa makini na karibu na watoto wao ili
kubaini mabadiliko yao. Lakini kitu kingine kikubwa, nawataka wachukue
hatua za haraka wanapobaini watoto wamefanyiwa ukatili kama huu,”
alisema Kamanda huyo.
Aliwaonya watu wazima wenye tabia hizo kuacha mara moja.
0 comments:
Chapisha Maoni