Vikosi
vya ulinzi na usalama vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la
Polisi na Magereza vimeungana kufanya mazoezi jana mjini Dodoma kwa
lengo la kuwa tayari zaidi kudhibiti uhalifu.
Akizungumza
wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto
alisema kuwa mazoezi hayo ya pamoja ni hatua ya kujiweka sawa
kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na wakati wowote.
Kamanda Muroto ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejitokeza kutaka kuharibu amani ya nchi atadhibitiwa kwa mujibu wa sheria.
Naye
Kaimu Kamanda wa kikosi cha JWTZ, Ihumwa, Kanali Mtukusya alisema kuwa
mazoezi hayo ni endelevu na kwamba ushirikiano huo utasaidia kuthibiti
vitendo vya uhalifu.
“Hauwezi
ukafanikisha kufanya kazi yako kwenye kitengo chako bila kuwa na
mahusiano na chombo kingine. Nina imani kwamba haya mazoezi haitakuwa
mwisho, tutaongea na makamanda wenzangu hapa ili tuone ni kitu gani
kingine tunaweza kufanya kuendeleza ushirikiano kwa vyombo vyetu vya
ulinzi na usalama,” alisema Kanali Mtukusya.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo, Dkt. Bilinith Mahenge
amesema kuwa hatua hiyo itasaidia upatikanaji wa taarifa za uhalifu kwa
haraka kwa kuwashirikisha wananchi.
“Kwa
sababu kama ataonekana mhalifu ambaye aliyetakiwa kumkamata ni polisi
lakini uliyemuona ni wewe afisa magereza basi hakikisha unatoa taarifa
kwa anayehusika ili aweze kushughulikiwa mara moja,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni